Showing posts with label HABARI ZILIZOTUFIKIA. Show all posts
Showing posts with label HABARI ZILIZOTUFIKIA. Show all posts

Sunday, 19 January 2020

Ujerumani yaandaa mkutano wa kilele kutafuta amani ya Libya


Libyen | Bundesaussenminister Heiko Maas trifft General Chalifa Haftar (imago images/photothek/X. Heinl)


Viongozi wa ulimwengu wanakusanyika mjini Berlin leo Jumapili kujadili mpango mpya wa amani ya nchini Libya. Mkutano huo wa kilele unalenga kuumaliza mzozo katika nchi hiyo na kuiepusha kugeuka kuwa "Syria ya pili".

Wadau muhimu wanakutana Jumapili mjini Berlin kujadili makubaliano ya kusitisha mapigano nchini Libya yanayoyumba. Wakati huo huo washiriki kwenye mkutano huo wanataka kutafuta njia ya kukabiliana na nchi za kigeni zinazoingilia kati masuala ya nchi hiyo inayokumbwa na machafuko tangu kuzuka ghasia za kuipinga serikali za mwaka 2011 zilizoungwa mkono na nchi wanachama wa jumuiya ya kijeshi NATO.
Ujerumani na Falme za Kiarabu (UAE) zimetoa wito wa pamoja kwa pande zote katika mzozo wa Libya kuzingatia makubaliano yaliyofikiwa ya kusitisha mapigano ya muda mrefu na kwa vikosi vya kigeni kuondoka nchini humo.
Msemaji wa serikali ya Ujerumani Steffen Seibert amesema wito huo ulitolewa baada ya kufanyika mkutano kati ya Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na mwanamfalme wa Abu Dhabi Sheikh Mohammed bin Zayed al Nahyan, kabla ya mkutano wa kilele kuhusu amani ya Libya ambapo viongozi wa kimataifa wanakutana mjini Berlin mnamo Jumapili 19.
Viongozi hao wawili wamesisitiza kwamba mzozo wa Libya hauwezi kutatuliwa kwa njia za kijeshi, bali kwa kudumisha amani na utulivu ambavyo vitafikiwa kwa njia ya mazungumzo. Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan amesema Falme za Kiarabu zingefanya kila jitihada kusaidia utekelezaji wa matokeo ya mkutano wa Berlin kuhusu Libya.
UAE ni mmoja wa washirika muhimu zaidi wanaomuunga mkono kiongozi wa waasi jenerali Khalifa Haftar ambaye vikosi vyake vinadhibiti sehemu kubwa ya Libya na wanaipinga serikali ya Waziri Mkuu Fayez al-Serraj iliyopo katika mji mkuu wa Libya, Tripoli inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.

Thursday, 16 January 2020

Naibu Waziri wa Madini Ladslausi Nyongo Ataka Wafanyabiashara Wa Madini Wasikamatwe Kamatwe Hovyo


Arusha
NAIBU Waziri wa Madini Ladslausi Nyongo  amepiga marufuku tabia ya  kamatakamata ya   wafanyabiashara wa madini nchini waliohifadhi  madini maeneo  wanayotaka kwa mujibu wa sheria.
 
Aidha katika kipindi cha mwaka wa fedha 2018/2019 Mkoa wa Arusha umekusanya  zaidi ya Sh.bilioni  30 zinazotokana na madini ya Vito ya aina mbalimbali.
 
Akizungumza jana Jijini Arusha wakati akifungua mkutano wa Mabalozi wa China nchini Tanzania na Tanzania nchini China pamoja na wafanyabiashara wa madini nchini,Naibu Waziri Nyongo alisema sheria inaruhusu wafanyabiashara kukaa na madini ili mradi wafuate sheria.
 
“Lakini siku za karibuni kumezuka tabia ya kusumbua wafanyabiashara waliofuata sheria za kukaa na  madini kwa kulipa kodi zote wanazotakiwa ili wakauze mahali popote wanapotaka,lakini wanasumbuliwa kwa kukamatwa na vyombo vya ulinzi,”alisema.
 
Alisema ili kuondoa mkanganyiko huo Wizara imejipanga kuelemisha wadau wa madini vikiwemo vyombo vya ulinzi na usalama kuhusu sheria za madini ikiwemo inayoruhusu wafanyabiashara hao kushikilia madini kabla ya kuuza kwenye soko za madini zilizopo.
 
Aidha aliomba Mabalozi wa China nchini Tanzania na yule wa Tanzania nchini China kuja kuwekeza nchini kwenye uwekezaji wa uongezaji thamani masini chini ya Gramu mbili ambayo yanaruhusiwa kwenda nje ya  nchi bila kuonhezwa thamani.
 
“Kama mnateknolojia ya kuongeza thamani madini haya tunawaalika mje kuwekeza ili tusiyatoe nje bila kuongeza thamani,”alisema.
 
Mkuu wa Mkoa Arusha Mrisho Gambo alisema wameleta mkutano huo ili kuongeza fursa kwa wafanyabiashara katika kupanua wigo wa soko la madini.
 
Alisema nchi ya Tanzania ina madini mengi lakini mchango wake kwa pato la Taifa ni asilimia 5.07 tofauti na pato la sekta ya utalii asilimia  17 na asilimia 25 katika kuingizia Taifa fedha za kigeni.
 
“Mchango huu hautoshi hivyo tumeamua kutumia mkutano huu ili tuongeze fursa katika madini na kukuza zaidi pato la sekta hii,”alisema.
 
Kuhusu ukusanyaji wa madini alisema yanatokana na soko la madini Namanga kukusanya Sh.bilioni 1.7  ya  madini ya vito na soko la Arusha walikusanya Sh.bilioni 34.46 katika kipindi cha Juni 2019 hadi Desemba 2019.
 
Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof.Idrisa Kikula aliomba  Ofisa Madini Mkazi wa Mikoa yote kukaa pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama kuelimishana sheria za madini ili wafahamu jinsi ya kudhibiti utoroshaji wa madini.
 
Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki aliomba wafanyabiashara kutumia fursa ya mkutano huo kuongeza mapato ya madini kutoka Sh.bilioni 500 ya sasa hadi kufikia Sh.Trioni moja.
 
“China wanunuzi wakubwa wa dhahabu  kama mwaka jana 2019 walinunua dhahabu tani 1506 hiki sio kiwango kidogo na hata madini mengine wananunua sana hivyo tujitahidi kuongeza fursa za soko nchini China,”alisema.

Wednesday, 15 January 2020

Rais wa Iran azihimiza nchi za kikanda kuvifukuza vikosi vya Marekani



Rais Hassan Rouhani wa Iran amesema nchi za kanda ya Mashariki ya Kati zinapaswa kuvifukuza vikosi vya jeshi la Marekani kutoka kwenye kanda hiyo.

Rais huyo ameyasema hayo alipokutana na waziri mkuu wa Syria Bw. Imad Khamis ambaye yupo ziarani nchini Iran. 

Amesema nchi za kanda hiyo zinapaswa kujitahidi kumaliza uwepo wa vikosi vya Marekani, na kuwafukuza wakaliaji kutoka kanda hiyo.

Bw. Khamis amesema uwepo wa vikosi vya Marekani nchini Syria ni mfano mzuri wa ukaliaji, na nchi za kanda hiyo zinapaswa kujitokeza kupinga uwepo haramu wa vikosi vya Marekani katika kanda hiyo.

Saturday, 8 December 2018

WAFANYAKAZI 93 WA ACACIA WAJENGEWA UWEZO KUSHIKA NYADHIFA ZA UONGOZI SEKTA YA MADINI

Wafanyakazi 93 wa kampuni ya ACACIA wakopatiwa mafunzo ya kushika nyadhifa za uongozi sekta ya madini, wakisikiliza utaratibu wa namna ya kusheherehekea mahafali ya kumaliza mafunzo hayo kwenye hoteli ya Malaika jijini Mwanza Desemba 7, 2018. Mgeni rasmi katika mahafali hayo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Nyangh'wale, Mhe.Hamimu Gwiyama.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Acacia waliotunukiwa vyeti vyao, kutoka kushoto, Bw. Fikiri Juma, Bw. Julius Maduhu na Bw.Emmanuel Nungu Wisaka, wakionyesha vyeti vyao baada ya kutunukiwa.

Bw. Hamimu Gwiyama, Mkuu wa Wilaya ya Nyangh'wale, akitoa hotuba yake. 








Bw. Hamimu Gwiyama, Mkuu wa Wilaya ya Nyangh'wale, akitoa hotuba yake.