![]() |
Add caption |
Muungano
wa Afrika (AU) umeionya Burundi dhidi ya hatua zinazoweza kuhujumu
mchakato wa amani baada ya kutolewa waraka wa kimataifa kumkamata rais
wa zamani Pierre Buyoya na maafisa wengine 16.
Wanatuhumiwa
kwa mauaji ya mwaka 1993 ya rais wa kwanza aliyechaguliwa nchini humo
ambaye alitoka kabila la Hutu, ambapo kuuliwa kwa, Melchior Ndadaye
kulisababisha kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Aidha,
kuna hofu kuwa kumlenga Buyoya ambaye ni kutoka kabila la Tutsi
anayeishi nchini Mali kunaweza kuchangia kuzuka misukosuko ya kikabila.
Zaidi
ya watu 300,000 waliuawa kwenye vita ya miaka 12 vya wenyewe kwa
wenyewe kati ya jeshi lenye watutsi walio wachache na waasi wa Hutu.
Hata
hivyo, Buyoya 69, alihusika kwenye mchakato wa amani uliomaliza vita
vya wenyewe kwa wenyewe na kuongoza kuchaguliwa kiongozi wa zamani wa
waasi wa Hutu, Pierre Nkurunziza kuwa rais mwaka 2005.
No comments:
Post a Comment