Mbowe, ambaye pia ni Mbunge wa Hai, sawa na Matiko wa Tarime Mjini, wamekata rufaa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam chini ya hati ya dharura wakipinga uamuzi wa Mahakama ya Kisutu kuwafutia dhamana katika kesi ya jinai inayowakabili mahakamani hapo.

Walifutiwa dhamana na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, anayesikiliza kesi hiyo Novemba 23 kutokana na maombi ya upande wa mashtaka yaliyodai wameshindwa kuhudhuria mahakamani wakati kesi yao ilipopangwa kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali bila sababu za msingi.
No comments:
Post a Comment