Kamishina wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa
nchini Tanzania,Mhe. Balozi Omari Ramadhani Mapuri amefungua mkutano wa
wa Tume na Wadau wa Uchaguzi katika mkoa wa Shinyanga kwa lengo la
kupeana taarifa kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.
Mkutano huo umefanyika leo Alhamis
Agosti 15,2019 katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga na
kuhudhuriwa na mkurugenzi wa uchaguzi,mratibu wa uandikishaji wa
mkoa,viongozi wa dini,vyama vya siasa,wawakilishi wa watu wenye
ulemavu,vijana,wanawake,asasi za kiraia,watendaji wa tume na waandishi
wa habari.
Balozi Mapuri alisema lengo la mkutano
huo ni kupeana taarifa kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga
kura ulioanza kwa awamu ya kwanza tarehe 18 Julai,2019 katika mikoa ya
Kilimanjaro na Arusha.
Alisema uzinduzi rasmi wa zoezi la
uboreshaji wa daftari la wapiga kura ulifanyika Mjini Moshi Julai 18
ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa na kwamba katika mkoa wa Shinyanga
uboreshaji wa daftari la wapiga kura utafanyika Agosti 26 hadi Septemba
1,2019.
"Lengo la kukutana nanyi leo ni
kuwafahamisha kuwa tume imekamilisha maandalizi ya zoezi la uboreshaji
wa daftari la kudumu la wapiga kura,ikiwemo uhakiki wa vituo vya
kujiandikisha,uandikishaji wa majaribio,maandalizi ya vifaa vya
uboreshaji wa daftari,maandalizi ya vifaa vya uboreshaji na mkakati wa
elimu ya mpiga kura naamini mafanikio ya zoezi hili yanategemea nyinyi
wadau",alieleza.
"Tume inatarajia kuanza uboreshaji wa
daftari la wapiga kura kwa awamu ya nne katika mikoa ya Mwanza
(halmashauri ya wilaya Kwimba),mkoa wa Shinyanga na mkoani Geita
(Halmashauri ya Mji wa Geita,Nyang'wale,Bukombe na Mbogwe) kuanzia
Agosti 26 hadi Septemba 1,2019",aliongeza.
Alifafanua kuwa uboreshaji wa daftari la
wapiga kura unafanyika kwa kutumia teknolojia ya kielektroniki ya
Biometriki (BVR) ambayo huchukua taarifa za kibaiolojia za mtu na
kuzihifadhi katika Kanzidata(Database) kwa ajili ya utambuzi.
"Uboreshaji wa daftari la wapiga kura
wa safari hii hautahusisha wapiga kura walioandikishwa kwenye daftari
la kudumu la wapiga kura mwaka 2015 ambao kadi zao hazihitaji
marekebisho yoyote ya taarifa.Uboreshaji huu utawahusu wapiga kura wapya
ambao wametimiza umri wa miaka 18 na wale ambao watatimiza umri wa
miaka 18 siku ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.",alisema Balozi Mapuri.
Alisema uboreshaji huo pia utahusisha
watu ambao wamehama kutoka maeneo yao ya awali na kuhamia maeneo mengine
ya uchaguzi na wale ambao kadi zao zimeharibika au kupotea na wale
ambao wanatakiwa kufutwa kwenye daftari baada ya kupoteza sifa wakiwemo
waliofariki dunia.
Kwa upande wake, Afisa Tehama Mwandamizi
kutoka Tume ya Uchaguzi ya Taifa, Frank Mhando aliwataka watu wenye
sifa ya kujiandikisha wajitokeze kwa wingi ili waandikishwe na
wanaohitaji kuboresha taarifa zao wakati ndiyo huu.
Alisema kila chama cha siasa kina wajibu
wa kuweka wakala kwenye kituo cha uandikishaji daftari la wapiga kura
huku akikisisitiza kuwa wakala hapaswi kuingilia majukumu ya tume ya
uchaguzi na kwamba yeyote atakayeleta masuala ya siasa kwenye vituo
atachukulia hatua.
Aliwataka wanasiasa kuepuka kufanya
siasa kwenye vituo bali majukumu yao yawe ni kuwatambua wenye sifa ya
kujiandikisha wapate sifa ya kupiga kura wakati wa uchaguzi.
"Hakuna uchaguzi bila wapiga
kura,hakuna kupiga kura bila kujiandikisha,niwaombe wanasiasa mhamasishe
watu wajitokeze kwenda kujiandikisha ili wawe na sifa ya kupiga kura",aliongeza.
ANGALIA PICHA
Kamishina wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa
nchini Tanzania,Mhe. Balozi Omari Ramadhani Mapuri akifungua mkutano wa
Tume na Wadau wa Uchaguzi katika mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kupeana
taarifa kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura leo katika
ukumbi wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Kamishina wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa
nchini Tanzania,Mhe. Balozi Omari Ramadhani Mapuri akifungua mkutano wa
Tume na Wadau wa Uchaguzi katika mkoa wa Shinyanga.
Afisa Tehama Mwandamizi kutoka Tume ya Uchaguzi ya Taifa, Frank Mhando mkutano wa Tume na Wadau wa Uchaguzi katika mkoa wa Shinyanga.
Afisa Tehama Mwandamizi kutoka Tume ya
Uchaguzi ya Taifa, Frank Mhando akiwataka watu wenye sifa ya
kujiandikisha wajitokeze kwa wingi ili waandikishwe kwenye daftari la
wapiga kura.
No comments:
Post a Comment