Washiriki wa Mashindano ya Mbio za
Morogoro Marathoni akiwemo Mgeni rasmi Mkuu wa mkoa wa Morogoro wakiwa
wamejiapnga tayari kuanza mbio za Kilometa 21 zilizoanzia jirani na
ofisi ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro.
Kikundi cha Mazoezi cha Mzimuni Jogging
Club wakiwa katika maandalizi ya kushiriki mbio hizo ambazo zimefanyika
kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Morogoro.
Kundi la Arusha Runners pia walikuwa ni washiriki wa tukio hilo .



Mshindi wa kwanza katika Mashindano Mapya ya Morogoro Marathon ,Amina
Mohamed akimaliza mbio za Kilometa 21 kwa kutumia saa 1:21:47
akimshinda mpinzani wake ,Rozalia Fabian
Mwanariadha Mkongwe Dickson Marwa akimaliza Mbio za Km 21 katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.
Baadhi ya Washiriki mbalimbali wakimaliza Mbio hizo katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.
Mgeni rasmi katika Mashindano hayo,Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro ,Kebwe Stephen Kebwe akizungumza kabla ya kukabidhi
zawadi kwa washindi wa Mbio za Morogoro Marathoni.
Baadhi ya Washiriki wa Mbio hizo wakimsikiliza Mgeni Rasmi katika Mashindano ya Mbio za Morogoro Marathoni .
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro Kihanga akizungumza katika Mashindano hayo.
Mgeni rasmi katika Mashindano ya mchezo wa Riadha ya Morogoro Marathon
,Mkuu wa mkoa wa Morogoro ,Kebwe Stephen Kebwe akimkabidhi mshindi wa
kwanza wa mbio za km 21 kwa wanawake Amina Mohamed zawadi ya king'amuzi
cha DSTV.
Mgeni rasmi katika Mashindano ya mchezo wa Riadha ya Morogoro Marathon
,Mkuu wa mkoa wa Morogoro ,Kebwe Stephen Kebwe akimkabidhi mshindi wa
pili wa mbio za km 21 kwa wanawake Rozalia Fabian zawadi ya king'amuzi
cha DSTV.
Mgeni rasmi katika Mashindano ya mchezo
wa Riadha ya Morogoro Marathon
,Mkuu wa mkoa wa Morogoro ,Kebwe Stephen Kebwe akimkabidhi mshindi wa
tatu wa mbio za km 21 kwa wanawake Monica Nicolaus zawadi ya
king'amuzi
cha DSTV.
Mgeni rasmi katika Mashindano ya mchezo wa Riadha ya Morogoro Marathon
,Mkuu wa mkoa wa Morogoro ,Kebwe Stephen Kebwe akimkabidhi mshindi wa
kwanza wa mbio za km 21 kwa wanaume ,Marko Joseph zawadi ya king'amuzi
cha DSTV.
Mgeni rasmi katika Mashindano ya mchezo
wa Riadha ya Morogoro Marathon
,Mkuu wa mkoa wa Morogoro ,Kebwe Stephen Kebwe akimkabidhi mshindi wa
tatu wa mbio za km 21 kwa wanaume Faraja Lazaro zawadi ya king'amuzi
cha DSTV.

Na Dixon Busagaga,Morogoro.
WANARIADHA Marko Joseph wa Singida na Amina Mohamed wa JKT –Arusha
jana wamewek rekodi mpya baada ya kufanikiwa kushika nafasi ya kwanza kwa mbio
za kilometa 21 kwa wananume na wanawake katika mashindano ya Mbio mpya za
Morogoro Marathon 2018.
Joseph alifanikiwa kushika nafasi hiyo baada ya kutumia saa
1:05:50 akifuatiwa na mwanariadha Faraja Lazaro w JKT –A rusha aliyemaliza mbio hizo zilizoanzia na
kumalizikia katika uwanja wa Jamhuri akituia saa 1:0:04.
Nafasi ya tatu imechukuliwa na mwanariadha mkongwe Dickson
Marwa aliyemaliza mbio hizo kwa kutumia saa 1:07:42 huku nafasi ya nne
ikichukuliwa na mwanariadha Anthony Moya aliyemaliza mbio kwa kutumia saa
1:07:42.
Kwa upande wa wanawake Amina Mohamed amefanikiwa kushika
nafasi ya kwanza baada ya kutumia saa 1:21:47 akifuatiwa n Rozalia Fabiani
liyemaliza mbio kwa kutumia saa 1:23:59 huku Monica Nicolaus akishika nafasi ya
tatu kwa kutumia saa 2:00:08.
Washindi wa Mbio za Kilometa tano wametangazwa Hashim
Athuman (18:50:07) kwa upande wa wanaume huku kwa wanawake akishika nafasi ya
kwanza Rosemary Mustapha kutoka mjini
Magharibi Zanzibar (23:41:66).
Nafasi ya pili kwa wanaume ni Mathayo Jeremia (Dar es
Salaam), kwa wanawake niNeema Masoud wa JKT-Arusha huku nafas ya tatu kwa
wanaume ikichukuliwa na Elias Maayunga na kwa wanawake ni Vaireth Kidosi.
Washindi katika mashindano hayo yanayoandaliwa na taasisi ya
Itete Sports Agency walikabidhiwa zawadi zao na Mkuu wa mkoa wa Morogoro ,Kebwe Stephen
Kebwe aliyekuwa mgeni rasmi ambaye pia alishiriki mbio za Kilometa tano.
Washindi kwa nafasi ya kwanza kwa mbio za kilometa 21 kwa
wanaume na wanawake wamejishindia fedha taslimu kiasi cha sh 400,000 na king’amuzi
cha DSTVkutoka kampuni ya Mult choice ambayo ilikuwa moja wa wadhamini wa mbio
hizo.
Washindi wa pili kwa mbio za km 21 wamejinyakulia kiasi cha
Sh 250,000 pamoja na king’amuzi cha DSTV huku washindi wa tatu wakijinyakulia
kiasi cha Sh 100,000 pamoja na king’amuzi cha DSTV huku washiriki wengine wakiambulia zawadi za Medali .
No comments:
Post a Comment