Tuesday, 14 January 2020

Polisi wamekanusha kupiga risasi waandamanaji wenye ghadhabu

Polisi nchini Iran katika mji mkuu Tehran, wamekanusha kutumia silaha dhidi ya waandamanaji walioghadhabishwa na kudunguliwa kwa ndege ya Ukraine.
Maafisa wa polisi walikuwa wamepata maagizo ya kuonyesha kwamba wao imara, mkuu wa polisi amesema.
Video zilizowekwa kwenye mitandao ya kijamii Jumapili, zilirekodi kile kilichoonekana kama maafisa wakifyatua risasi pamoja na mwanamke aliyejeruhiwa akibebwa.
Maandamano yalianza Jumatatu baada ya Iran kukubali kwamba ilirusha kombora kimakosa dhidi ya ndege ya abiria ya Ukraine na kuanguka karibu na Tehran.


Watu wote 179 waliokuwa kwenye ndege hiyo PS752, wengi wao wakiwa raia wa Iran na Canada walikufa.
Awali, raia wa Iran walikuwa wameungana kuomboleza kifo cha Jenerali Qasem Soleimani, ambaye alikuwa wa pili mwenye madaraka makubwa nchini humo, baada ya kushambuliwa na ndege ya Marekani isiyokuwa na rubani nchini Iraq.
Taarifa za hivi karibuni zinaonesha uwezekano wa kutokea kwa maandamano zaidi sawa na yaliyoshuhudiwa Novemba mwaka jana dhidi ya kupanda kwa bei ya mafuta. Makundi ya haki za binadamu yanasema mamia ya watu waliuawa.
ShambulioNini kilitokea katika maandamano ya wikiendi?
Maandamano yaliyotokea Jumapili yaliendelea hadi usiku wa manane huku watu wakiendelea kupandwa na ghadhabu dhidi ya serikali ya Iran na vikosi vya ulinzi vilivyodungua ndege ya Ukraine.
Video iliyowekwa kwenye mtandao wa kijamii inaonesha waandamanji wakiipiga mateke na kuangusha bango kubwa la Soleimani.

No comments:

Post a Comment