Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Mafunzo kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu
Tawala wa Mikoa kwenye ukumbi wa Hazina jijni Dodoma, Desemba 3, 2018.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi
ya Makatibu Tawala wa Mikoa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
wakati alipofungua Mafunzo kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa
Mikoa kwenye Ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Desemba 3, 2018. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi
ya Wakuu wa Mikoa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati
alipofungua Mafunzo kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa
kwenye Ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Desemba 3, 2018. (Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,
Paul Makonda baada ya kufungau Mafunzo kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu
Tawala wa Mikoa kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Desemba 3,
2018. Wengine pichani kutoka kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
TAMISEMI, Selemani Jafo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi,
Profesa Joseph Semboja, Waziri Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst.), George Mkuchika na
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Josephat Kandege. (Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya Wakuu wa Mikoa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua Mafunzo kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa kwenye Ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Desemba 3, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu,Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Mikoa
baada ya kufungua Mafunzo kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa
kwenye Ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Desemba 3, 2018. (Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu,Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Tawala wa
Mikoa baada ya kufungua Mafunzo kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala
wa Mikoa kwenye Ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Desemba 3, 2018. (Picha
na Ofisi ya Waziri Mkuu)
NA OWM, DODOMA
*Mfunzo hayo yatawasaidia kusimamia utumishi na kuzingatia miiko ya uongozi
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefungua mafunzo kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa, ambapo amesema baada
ya mafunzo hayo Serikali inatarajia watasimamia kikamilifu nidhamu
katika utumishi wa umma na wao wenyewe watakuwa kioo katika kuzingatia
miiko ya utumishi wa umma.
Kadhalika,
Waziri Mkuu amesema viongozi hao wa mikoa watazingatia kikamilifu
mipaka ya madaraka yao na kwamba hatua watakazozichukua katika uongozi
na utendaji wao zitazingatia sheria, kanuni na taratibu zilizopo nchini.
Waziri
Mkuu amefungua mafunzo hayo yanayoendeshwa na Taasisi ya Uongozi leo
(Jumatatu, Desemba 3, 2018) katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma,
ambapo pamoja na mambo mengine amewataka wakasimamie kikamilifu
mapambano dhidi ya madawa ya kulevya.
“Mkadumishe
uhusiano mwema baina yenu na watumishi walio chini yenu, kwa kuzingatia
kuwa kila mtumishi anao mchango katika kuboresha utendaji kwenye kituo
chake cha kazi. Nina matarajio makubwa kuwa mtadumisha uhusiano mzuri
kikazi na viongozi wa juu na pia uhusiano wa diplomasia ya heshima na
viongozi wengine ndani ya mihimili yetu mitatu.”
Hata
hivyo, Waziri Mkuu amewataka viongozi hao wahakikishe kila mmoja wao
anaandaa mpango kazi unaoainisha shughuli zake za kila siku. “Mkuu wa
Mkoa, Katibu Tawala wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi na Wakuu wa
Idara wote na Watumishi wote wawe na mpango kazi wa utekelezaji wa
majukumu yao.”
Amesema
viongozi hao wanatakiwa wasimamie nidhamu kazini na uwajibikaji wa
watumishi kwa wananchi, ambapo pia amewasihi watende haki kwa wananchi
na watumishi walio chini yao. Pia lazima watumishi wa Serikali wawapokee
na kuwahudumia wananchi kwa staha, wawasikilize kero zao na kuzitafutia
ufumbuzi.
Waziri
Mkuu amesema viongozi hao wanatakiwa waendelee kusimamia amani na
utulivu kwenye mikoa yao ili watu waendelee kufanya shughuli zao bila
wasiwasi wowote kwani amani na utulivu ndiyo itawawezesha nchi iendelee
kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje.
“Tunakumbushwa
sisi viongozi tuhakikishe tunaziendeleza rasilimali za nchi hii kwa
faida ya Watanzania wote bila kubagua jinsia, kabila, dini, rangi ya
ngozi, mtu atokako ndani ya nchi
ilimradi hajavunja sheria; wala ubaguzi mwingine wa aina yoyote. Tunaaswa tuwahudumie Watanzania wote kwa usawa.”
Kuhusu
mada zitakazowasilishwa kwenye mafunzo hayo, Waziri Mkuu amesema
zitawawezesha viongozi hao kupata fursa ya kutafakari na kujitathmini
kuhusu hatua za kujiimarisha zaidi kiuongozi na kiutendaji. “Hatua hizo
ni lazima ziwe pamoja na kubadilika kwa mtazamo na kujirekebisha endapo
mtabaini maeneo mliyokuwa mkikosea tangu mlipokabidhiwa ofisi hadi
sasa.”
Waziri Mkuu amesema mada zitakazowasilishwa kwenye mafunzo hayo zinahusu majukumu na mipaka ya kazi,ambapo
watajifunza namna ya kufanya kazi bila mikwaruzano isiyo na tija baina
yao na viongozi wa mihimili mingine ya dola, viongozi wa kisiasa na
watendaji wengine Serikalini.
Amesema mada nyingine inahusuuongozi,
hisia na mahusiano mahali pa kazi, ambapo itawawezesha kujiimarisha
katika mbinu za kuwaongoza watumishi walio chini yao kwa kujenga na
kudumisha mshikamano na ushirikiano wa pamoja.
“Mada
itafafanua pia namna mnavyotegemeana na watumishi wa kada na ngazi
mbalimbali katika kutimiza majukumu yenu. Ni muhimu sana kufanya kazi
kama timu moja ili muweze kuyafikia malengo ya taasisi kwa upana wake na
si malengo ya mtu au kiongozi mmoja.”
Amesema
kwenye mada inayohusu muundo wa Serikali na namna inavyofanya kazi
watauelewa vizuri zaidi muundo wa Serikali ulivyo na jinsi unavyofanya
kazi. Pia wataielewa vizuri zaidi itifaki na kuheshimiana kwa ngazi
mbalimbali kutoka Waziri, Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya, Makatibu Tawala,
Wakurugenzi, Wakuu wa Idara hadi Wananchi.
Kwa upande wake,
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Profesa Joseph Semboja
amesema mafunzo hayo ya wiki moja yatajikita katika maeneo makuu matatu
ambayo ni kuimarisha uwezo wa washiriki katika kufanya maamuzi ya
kimkakati yanayozingatia mahitaji na manufaa mapana ya sasa na ya baadae
kwa jamii. Ametaja
eneo la pili kuwa ni kuimarisha uwezo wa washiriki katika kuongoza
rasilimali watu na kusimamia rasilimali nyingine ili kutekeleza
kikamilifu na kwa mafanikio maamuzi ya kimkakati waliyoyafanya katika
kipengele cha kwanza. “Eneo
la tatu ni la kuimarisha uwezo wa washiriki katika kujijengea sifa
binafsi za uongozi ili awe na ushawishi kwa wananchi anaowaongoza. Hili
ni jambo la msingi, kiongozi mwenyewe awe mfano bora wa kuigwa. Awe
muadilifu, mtenda haki, mfuata sheria na taratibu pamoja na kufahamu na
kuheshimu miiko ya uongozi.” Mafunzo
hayo yamehudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Selemani
Jafo. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala
Bora, Kapteni Mstaafu, George Mkuchika, Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge na Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Josephat Kandege pamoja na maafisa wengine wa Serikali.
No comments:
Post a Comment