Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akizungumza na waandishi wa habari katika
ukumbi wa CBT Mkoani Mtwara kutoa ufafanuzi juu hali ya ununuzi wa
korosho Tarehe 3 Disemba 2018. (Picha Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo)
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Mtwara
Timu
ya wataalamu wa Uhakiki wa wakulima wa Korosho imeongezeka katika mikoa
ya Mtwara, Lindi na Ruvuma kutoka 11 mpaka kufikia timu 20 ili kuongeza
uharaka wa uhakiki kwa ajili ya malipo ya wakulima.
Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga ameyasema hayo tarehe 3 Disemba 2018
wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa CBT Mkoani
Mtwara kutoa ufafanuzi juu hali ya ununuzi wa korosho.
Katika
mkutano huo pia Waziri Hasunga amesema kuwa timu ya wataalamu tayari
imewasili mkoani Pwani kwa ajili ya kuanza uhakiki wa wakulima wa
korosho kuanzia leo tarehe 3 Disemba 2018 ambapo mkoa wa Pwani utakuwa
mkoa wanne kuhakikiwa ukiungana na mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma.
Alisema
kuwa hadi kufikia tarehe 1 Disemba 2018 jumla ya vyama vya ushirika 212
vilikwisha hakikiwa kati ya vyama 504 vilivyopo katika mikoa hiyo
mitatu ya kusini.
Aidha, Vyama 157 vimekwishalipwa fedha zao kati ya vyama 617 vinavyojihusisha na korosho nchini.
Mhe
Hasunga alisema kuwa tayari Bilioni 35,540,709,854 zimekwishalipwa kwa
wakulima wa korosho ambapo kilo Milioni 10,769 za korosho
zimekwishalipiwa.
Mhe Hasunga ameviambia vyombo vya habari kuwa idadi ya wakulima ambao wameshalipwa mpaka tarehe mosi Disemba ni wakulima 34,938
Amefafanua
zaidi kwa kusema kuwa katika mkoa wa Lindi tayari Bilioni 12.7
zimelipwa ilihali katika Mkoa wa Ruvuma ni Bilioni 4.9 na Mkoa wa Mtwara
ni Bilioni 17.9
No comments:
Post a Comment