Katibu
Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amemsifia Waziri Mkuu wa zamani, Edward
Lowassa akisema kuwa ni mtu muungwana na hana unafiki na kumtaka Bernard
Membe kuiga tabia hiyo.
Akizungumza
jana usiku Desemba 2, 2018 mjini Geita Bashiru amesema Lowassa ambaye
kwa sasa ni mwanachama wa CHADEMA, hajawahi kuzusha wala kutoa kauli
mbaya dhidi ya Rais John Magufuli.
"Mtu
kubaki ndani ya CCM kinafiki na kuendelea kugawa chama kwa makundi
hawezi kumvumiliwa na nitahakikisha ninamaliza makundi kwenye chama",
amesema Dkt Bashiru.
Kauli
hiyo ya Dk. Bashiru ni mwendelezo wa mjadala kati yake na Membe,
aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, akimtaka
afike ofisini kwake kujieleza, ambapo alitoa kauli hiyo kwa mara ya
kwanza akiwa mkoani Geita, akijibu ujumbe uliotumwa kwenye akaunti ya
mtandaoni ya mtu mwenye jina la Bernard Membe kujibu tuhuma zilizotolewa
na Dkt. Bashiru akiwa Geita.
Dkt.
Bashiru alimtuhumu Membe kuandaa mpango wa kumkwamisha Rais John
Magufuli katika uchaguzi wa Rais na kwamba tangu ateuliwe hajawahi
kuonana na mbunge huyo wa zamani wa Mtama.
Dkt.
Bashiru amesema anamheshimu Lowassa kwa uamuzi wake wa kuondoka CCM
baada ya kutopewa ridhaa ya kugombea Urais na kwenda chama kingine
badala ya kubaki ndani ya chama tawala kinafiki na kuwagawa wanachama
Amesema hayupo tayari kuona migogoro iliyowakumba makatibu wakuu waliomtangulia wakati wa uchaguzi akutane nayo sasa na kwamba mkakati wake mkuu ni kuua makundi.
Amesema hayupo tayari kuona migogoro iliyowakumba makatibu wakuu waliomtangulia wakati wa uchaguzi akutane nayo sasa na kwamba mkakati wake mkuu ni kuua makundi.
No comments:
Post a Comment