Video
inayosambaa mtandaoni ikimuonyesha Naibu Spika wa Bunge, Dr. Tulia
Ackson Mwansasu akiwa na Wabunge wanzake wakiimba wimbo ‘Mwanza’ wa
muimbaji Rayvanny ambao umefungiwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA),
imezua gumzo mtandaoni.
Wabunge
hao walikuwa nchini Burundi kwenye michuano ya wabunge na baada ya
kuibuka na ushindi wakaanza kushangilia kwa style ya kuimba wimbo huo
ambao upo kifungoni.
Mbunge
wa Arusha Mjini, Godbless Lema amefunguka kwa kudai kwamba, Mhe Spika
Tulia anatakiwa kuhojiwa na kamati ya maadili ya Bunge kuhusiana na
tukio hilo.

No comments:
Post a Comment