Mahakama
ya Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, imemhukumu kifungo cha miaka mitatu
jela pamoja na kurejesha Sh milioni 10.3, Mwalimu Josiah Mkome baada ya
kukutwa na hatia katika kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa inamkabili.
Mwalimu
Mkome alikuwa akifundisha Shule ya Sekondari Kandawe wilayani Magu,
mkoani Mwanza alishtakiwa kwa kosa la kupokea mishahara miwili kutoka
katika Wilaya ya Magu na Maswa kinyume cha sheria.
Mwendesha
mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wa
Mahakama ya Wilaya ya Maswa, amedai mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama
hiyo Fredrick Lukuna, mshtakiwa alipokea mishahara hiyo miwili tangu
Februari mwaka 2012 hadi Mei mwaka 2015.
No comments:
Post a Comment