Nchi
mbili zenye uchumi mkubwa zaidi duniani wamekubaliana kufikia
masikilizano madogo katika vita iliyokuwa inaongezeka ya kibiashara
baada ya kukutana kwa marais Donald Trump na Xi Jinping katika mkutano
wa nchi tajiri zenye viwanda G20.
Trump
akiongea na waandishi wa habari katika ndege ya rais Air Force One
baada ya ndege kuondoka Argentina, amesema makubaliano yaliofikiwa
wakati wa chakula cha usiku na Xi, yatakuwa katika historia “kama moja
ya makubaliano makubwa yaliyowahi kufikiwa…Na yatakuwa na athari kubwa
chanya katika kilimo, bidhaa za viwandani na kompyuta – kila aina ya
bidhaa.”
Trump
amekubali kuwa ushuru wa bidhaa za China zenye thamani ya dola za
Marekani milioni 200 kuendelea kuwa asilimia 10, na hatoongeza ushuru
huo hadi asilimia 25, kwa hivi sasa, kama alivyokuwa ametishia
kutekeleza hilo ongezeko ifikapo Januari 1, kwa mujibu wa tamko la White
House.
Trump
na Xi pia “ wamekubaliana mara moja kuanza mazungumzo ya mabadiliko ya
miundo ya kuhamisha teknolojia, kulinda haki miliki za kitaaluma,
mazungumzo juu ya bidhaa zisizo kuwa na vikwazo vya ushuru, udukuzi wa
mitandao na wizi wa kimitandao, huduma na kilimo, kwa mujibu wa tamko la
White House.
“Pande
zote zimekubaliana kuwa wataendelea kufanya juhudi za kukamilisha
majadiliano haya katika kipindi cha siku 90. Na iwapo muda huu
utamalizika na pande hizi mbili hazijafikia makubaliano, ushuru huu wa
asilimia 10 utaongezeka hadi asilimia 25.
Baadhi
ya maelezo hayo yalifafanuliwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang
Yi, ambaye alithibitisha kuwa nchi zote mbili zitaanza mazungumzo.
No comments:
Post a Comment