Jeshi
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemuachia kwa dhamana Meya wa
Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita baada ya kumshikilia kwa zaidi ya
saa 24.
Mwita
ambaye ni diwani wa Vijibweni (Chadema) alikamatwa na polisi juzi
Desemba Mosi, 2018 saa 11 jioni baada ya kumaliza kikao cha kutunisha
mfuko wa vijana na kuachiwa jana saa 2 usiku akituhumiwa kufanya
maandamano bila kuwa na kibali.
Wakili
wa Meya huyo, Alex Massaba amesema baada ya polisi kuchukua maelezo
walimuachia kwa dhamana na kumtaka aripoti leo kwa mkuu wa upelelezi
Wilaya ya Kigamboni.
No comments:
Post a Comment