Waumini wa Kanisa la Sauti ya Uzima wamevamia na kushambulia kwa mawe nyumba ya Mchungaji wa Kanisa hilo, Nabii Elia (36) wakimtuhumu kuwa ni mshirikina.
Jina
kamili la Nabii Elia limeelezwa kuwa ni Elia Zabron Balashika raia wa
Burundi ambaye amekuwa akitoa huduma ya roho zaidi ya miaka sita eneo
hilo.
Akizungumza
na waandishi wa habari juzi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Damas
Nyanda alisema tukio hilo lilitokea Mtaa wa Kazima Ringini Manispaa
ya Mpanda, baada ya waumini kuvamia nyumbani kwa kiongozi huyo.
Alisema waumini watano wametiwa mbaroni na watu kadhaa kutokana na kujichukulia sheria mkononi.
Aliwataja
waumini waliokamatwa kuwa ni William Kaluzi (19) mkazi wa Mtaa wa
Nsemulwa , Steven Alfred (31) mkazi wa Mtaa Kazima, Nicholaus Shadrack
(33) mkazi wa Mtaa wa Kazima na Tekla Didas (17) mkazi wa Kijiji cha
Rungwa
Wengine
ambao siyo waumini wa kanisa hilo ni Mashaka Moshi (23) mkazi wa
Mtaa wa Nsemulwa na Faraja Hussein (22) mkazi wa Mtaa wa Kazima.
Kamanda
Nyanda alisema chanzo ni imani za ushirikina baada ya taarifa kuzagaa
kuwa Nabia Elia alikuwa ameweka ‘misukule’ watano nyumbani kwake
ambao waumini wa kanisa hilo walimtaka awatoe hadharani.
Alisema
siku ya tukio saa 11:30 jioni, Nabii Elia alifika Kituo cha Polisi
mjini Mpanda ambako alitoa taarifa kuwa nyumba yake ilikuwa imevamiwa
na wananchi ambao walikuwa wanaharibu mali zake .
“Ndipo
timu ya polisi wakiongozwa na SSP Focus Malengo, Mkuu wa Upelelezi wa
Makosa ya Jinai Mkoa wa Katavi, Abdallah Hussein na Kaimu Ofisa
Upelelezi Wilaya ya Mpanda, Mkaguzi Ngagala, walifika eneo la tukio na
kukuta kundi la wananachi wakiendelea kurusha mawe,“ alieleza.
Alisema
walianza kutuliza ghasia kwa kufyatua mabomu ya kishindo kuwatawanya
wananchi hao, huku waumini wawili wa kanisa hilo wakijeruhiwa kwa
kupigwa mawe kichwani .
Waliojeruhiwa
ni Mchungaji wa Kanisa hilo, Mussa Elia (24) na mkazi wa Mtaa wa
Kazima, Joseph Elia (29) ambao wanadaiwa kuwa ni ndugu zake na Nabii
Elia .
Alisema
mali za Nabii Elia zilizoharibiwa ni pamoja na vioo vinne vya
madirisha ya nyumba yake, kioo cha nyuma cha gari lake la Spacio, huku
thamani kamili ikiwa bado haijafamika.
No comments:
Post a Comment