
Jopo la mawakili wa rais wa Marekani Donald Trump kwa mara ya kwanza limetoa majibu rasmi kuhusiana na mashtaka dhidi yake likitaja kuwa "vita vikali" dhidi ya demokrasia.
Taarifa yao ilisema vifungu vya sheria kuhusu hoja ya kumuondoa rais havikutaja makosa yoyote yaliyofanywa na kuongeza kuwa ni ''njama'' ya jaribio la kuingilia uchaguzi wa urais wa mwaka 2020.
Kauli hiyo inakuja wakati Democrats wamewasilisha malalamishi yao kabla ya kuanza wa kesi hiyo wiki ijayo.
Bw. Trump ni rais wa tatu wa Marekani kukabili na mashtaka.
- 'Trump alijua mipango inayosukwa dhidi ya hasimu wake'
- Maseneta waapishwa kusikiliza kesi ya kumuondoa Trump madarakani
Anatuhumiwa kwa kutumia vibaya mamlaka yake na kuzuia bunge la Congress kufanya uchunguzi. Amepinga kufanya kosa lolote na kutaja kesi dhidi yake kuwa "owongo".
Bunge hilo linaloongozwa na chama cha upinzani cha Democrats, lilipiga kura ya kutokuwa na imani na rais mwezi uliopita.
Bunge la Seneti,linaloongozwa na chama cha Republican cha Bw. Trump, litaamua ikiwa atashitakiwa na kumuondoa madarakani.
Mawakili wa Trump walisema nini?
Katika stakabadhi ya kurasa sita jopo la mawakili wa rais waliwasilisha hoja wanazotarajia kutumia kama katika kesi hiyo.
Jopo hilo la wanasheria, linaloongozwa na wakili wa White House Pat Cipollone na wakili wa kibinafsi wa Bw. Trump Jay Sekulow, lilisema linapinga kesi ya kutaka kumuondoa rais madarakani kwa misingi ya kutofuata kanuni na ukiukaji wa katiba, likidai kuwa rais hakufanya kosa lolote na kwamba anaonewa.
Katika maelezo ya yaliyowasilishwa siku ya Jumamosi, Democrats walielezea kwa kina kwanini wanataka Bw. Trump aondolewe ofisini.
Walisema kuwa rais "alikiuka kiapo cha uaminifu wa kazi hatua ambayo ilihujumu imani ya wanaichi", na akutaja mwenendo wake kuwa "ndoto ya ajabu" kwa waanzilishi wataifa.
No comments:
Post a Comment