
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Semistocles Kaijage.
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Semistocles Kaijage, wakati akisoma risala ya
uchaguzi mdogo wa Udiwani unaohusisha kata za Miteja, Kivinje au Sigino ,
Somanga na Mitole katika Halmashauri ya Kilwa, kata ya Muhinda katika
Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe na Kata ya Nkoanekoli katika Halmashauri ya
wilaya ya Meru.
Wapiga Kura wapatao 31,818
wanatarajiwa kupiga Kura kuwachagua Madiwani katika Kata 6 za Tanzania Bara, na
uchaguzi huo utafanyika katika vituo 91 vya kupigia kura ambako ndipo wapiga
kura walijiandikishia kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na
Madiwani wa Mwaka 2015.
“Wananchi waheshimu Sheria za
Nchi wakati wote wa upigaji, kuhesabu, kujumlisha kura na kutangaza matokeo.
Pale panapokuwa na malalamiko yoyote ya ukiukwaji wa sheria na taratibu za
uchaguzi, yafikishwe kwenye mamlaka husika.”, Amesema Kaijage
Jaji Kaijage aliwataka wapiga kura
kuondoka kwenye maeneo ya kituo cha kupigia kura mara baada ya kupiga kura na
kujiepusha na mikusanyiko au mikutano katika maeneo ya vituo vya kupigia kura
kwani vyama vya siasa vimeweka mawakala vituoni ambao watalinda maslahi ya
vyama husika na wagombea wao.
“Ni wajibu wa vyama vya siasa
vinavyoshiriki katika uchaguzi kuweka mawakala katika vituo vyote vya kupigia
na Kujumlishia Kura kwa utaratibu ambao tulikubaliana na umekuwa ukitumika
katika chaguzi"
Maeneo mbalimbali yamekuwa yakifanya
uchaguzi kutokana na sababu za viongozi wake kujiuzulu wengine kupoteza sifa za
kuwa viongozi wa maeneo hayo kwa sababu za vifo au kufungwa.
Kwenye chaguzi za marudio vyama
mbalimbali vya upinzani ikiwemo CHADEMA, ACT, NCCR - Mageuzi vilitangaza
kususia kwa kile ilichokidai kuwa chaguzi hizo zimekuwa haziwatendei haki.
No comments:
Post a Comment