
Rais Magufuli na Uhuru Kenyatta
Hilo limewekwa wazi na Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga jijini
Arusha leo Disemba 1, 2018 ambapo amesema mchakato wa kukamilisha sarafu hiyo
unaendelea vizuri.
'Sisi wana Afrika Mashariki
tunaelekea kuinua uchumi wetu kwa ushirikiano ambapo hatua ya awali tunaanza na
kutumia sarafu ya pamoja ambayo itasaidia kwenye hili soko la pamoja
tunalolianzisha hivyo ifikapo mwaka 2020 tutakuwa na Umoja wa sarafu kwa
kutumia sarafu yetu'', amesema.
Aidha Balozi Mahiga ameweka wazi mipango
mbalimbali ya nchi hizo katika kukuza uchumi kwa kutaja maeneo ambayo
yanatakiwa kufanyiwa kazi ili kufikia lengo hilo la pamoja.
''Ili kupata maendeleo hapa duniani
ni lazima utashi wa kisiasa uwepo, kuondoa vikwazo vya biashara, vikwazo vya
mitaji baina ya nchi moja na nyingine pamoja na kupunguza vikwazo vya watu
wanaoshirikiana au kutembeleana kwa kuvuka mpaka wa nchi moja kwenda
nyingine'', ameongeza.
Mahiga na baadhi ya viongozi wa Nchi
za Jumuiya ya Afrika Mashariki wapo jijini Arusha ambako ulikuwa ufanyike
mkutano wa wakuu wa nchi za Jumuiya hiyo (EAC), lakini ukaahirishwa baada ya
nchi ya Burundi kukosa mwakilishi.
No comments:
Post a Comment