Mkuu wa MKoa wa Singida Dkt. Rehema
Nchimbi akifunga mafunzo maalum ya siku sita kwa wadau zaidi ya 300 kutoka katika mikoa mbalimbali nchini yaliyokuwa yameandaliwa na Baraza la Taifa la watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI (NACOPHA) kupitia “Mradi wa Hebu Tuyajenge” unaotekelezwa katika kipindi cha miaka mitano 2019-2024, unaofadhiliwa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) katika mikoa 22 Tanzania Bara. kushoto Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagisa, Kulia Mkurugenzi wa Utatifi wa NACOPHA Pantaleo Shoki
Nchimbi akifunga mafunzo maalum ya siku sita kwa wadau zaidi ya 300 kutoka katika mikoa mbalimbali nchini yaliyokuwa yameandaliwa na Baraza la Taifa la watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI (NACOPHA) kupitia “Mradi wa Hebu Tuyajenge” unaotekelezwa katika kipindi cha miaka mitano 2019-2024, unaofadhiliwa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) katika mikoa 22 Tanzania Bara. kushoto Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagisa, Kulia Mkurugenzi wa Utatifi wa NACOPHA Pantaleo Shoki
>Awataka wenye virusi kufanya kazi bila hofu
>Awaonya wanaomchokoza,asisitiza hatatia nia
Na John Mapepele
Mkuu wa Mkoa wa
Singida, Dkt. Rehema Nchimbi amempongeza Rais Magufuli kwa kuvunja
rekodi ya maendeleo kabla ya mwaka 2025 na kuifanya Tanzania kuingia
kwenye nchi za uchumi wa kati duniani Julai Mosi mwaka huu.
Huku akiwahimiza
watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI nchini kufanya kazi kwa bidii bila
kuwa na hofu sambamba na kumtanguliza Mungu na kutumia fursa za mikopo
inayotolewa na Serikali ya Awamu ya Tano ili ku kuinua hali za maisha
na kuongeza pato la taifa kwa ujumla
Dkt. Nchimbi
ameyasema hayo leo katika Mji Mdogo wa Manyoni mkoani Singida alipokuwa
akifunga mafunzo maalum ya siku sita kwa wadau zaidi ya mia 3 kutoka
katika mikoa mbalimbali nchini yaliyokuwa yameandaliwa na Baraza la
Taifa la watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI (NACOPHA) kupitia
“Mradi wa Hebu Tuyajenge”.
Mradi huo
unaotekelezwa katika kipindi cha miaka mitano 2019-2024,unaofadhiliwa
na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) katika mikoa
22 Tanzania Bara.
Amesema kwa sasa
Serikali ya Awamu ya Tano imepiga hatua kubwa ya kupiga vita unyanyapaa
dhidi ya watu wanaishi na virusi vya UKIMWI na kwamba watu wote wana
haki na fursa sawa mbele ya Serikali yao hivyo hakuna sababu ya wao
kuendelea kujinyanyapaa wenyewe na badala yake wawe walimu wa
kuwaelimisha wengine kwenda kupima na kutambua hali zao na kuendelea
kuchapa kazi ili kuinua uchumi wan chi yetu.
“Kubwa ndugu
zangu hapa ni kumtanguliza Mungu mbele, kutoa hofu na kuachana na
mambo yote ambayo yanapelekea kudhoofu kwa afya zetu kama vile unywaji
wa pombe hata kama wake zetu wanapika kwa ajili ya biashara na badala
yake tutumie juisi lishe za matunda ya asili kama vile Sasati, Ubuyu na
Ukwaju” amesisitiza Dkt. Nchimbi
Umewaelekeza
Wataalam wa Maendeleo ya Jamii wa Mkoa wa Singida kuangalia namna ya
kuja na mikakati madhubuti ya kiuendelevu ya kuwakopesha wanaoishi na
UKIMWI ili kuwaletea maendeleo huku akisisitiza kuwa Mkoa wake
utaendelea kutekeleza mikakati iliyojiwekea ya kuinua maisha ya
wanainchi wake ikiwa ni pamoja na mkakati wa kuwavusha salama mama na
mtoto.
Aidha ameweka
msimamo wake wa kutokuonesha nia yeyote ya kuomba ridhaa ya kugombea
Ubunge katika uchaguzi wa mwaka huu huku akiwaonya watu ambao wamekuwa
wakianza kudanganya kuwa atagombea ambapo alisisitiza kuwa nafasi hiyo
ya ukuu wa Mkoa aliyopewa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli ni ya
heshima kubwa.
“Naomba niliseme
hili, na tayari nimeshalisema mara kadhaa hata hivi karibuni
nilipokuwa nyumbani kwangu, kijijini Matufa, Babati Manyara nilipo
hudhuria mazishi ya mtoto wa Kaka yangu aliyefariki kwa ajali ya
Pikipiki kwamba nilikwenda kuungana na familia yangu katika msiba wa
kijana wetu na si vinginevyo. Ninaridhika sana na nafasi hii niliyo nayo
ya ukuu wa Mkoa” alisema Dkt. Nchimbi huku akishangiliwa na umati wa
wadau wa mafunzo hayo
Baadhi ya
waombolezaji wamesikika kupongeza msimamo wa kiongozi huyo, huku
wakisema kuwa Msimamo huo unapaswa kuigwa na viongozi wengine kwa kuwa
umejikita katika kuwaletea maendeleo wananchi badala ya kuwa na tamaa
za madaraka.
“Binafsi
nampongeza sana Mama Nchimbi kwani kwa muda wote amekuwa aking’ang’ana
na kuwaunganisha watu wote bila kujali dini wala rangi kwa, hata sisi
leo ametutia moyo sana kiasi kwamba baada ya kutoka hapa tumekuwa na
nguvu mpya ya kuchapa kazi na kushirikiana na Serikali yetu ya
kujiletea maendeleo Zaidi ili tutoke katika nchi za uchumi wa kati na
kwenda katika nchi tajiri duniani na tuna imani kubwa chini ya Rais wetu
Magufuli tutafika” amesema Amina Huredi ambaye ni Mshiriki wa mafunzo
hayo kutoka Singida
Mkurugenzi wa
Utatifi wa NACOPHA Pantaleo Shoki amemshukuru Mkuu wa Mkoa na
kumhakikishia kuwa wataendelea kushikiana na Serikali ili kuhakikisha
kuwa malengo ya Mradi huo yanatimia kama yalivyopangwa.
Shoki amesema
Mradi unalenga kufikia Mkakati wa Shirika la Umoja wa Mataifa la
Kupambana na UKIMWI(UNAIDS) wa 95-95-95 yaani asilimia 95 ya watu wote
wanaoishi na maambukizi ya VVU wawe wamepima na kugundua afya
zao,asilimia 95 ya watu wote waliopimwa na kukutwa na maambukizi wawe
wameanza tiba na asilimia 95 walio kwenye tiba wawe wamefubaza virusi
hivyo ifikapo 2030
No comments:
Post a Comment