Wadau wa Maendeleo kutoka Shirika la Maendeleao la Japan (JICA)wakiwa
katika mkutano wa Ushirikiano wa Kiufundi katika kuwezeshauboreshaji wa
Maendeleo ya Skimu za Umwagiliaji Chini ya Mpango wa Maendeleo ya Wilaya
Awamu ya Pili (TANCAID II) jijini Dodoma leo.
. Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Kamati ya Pamoja ya Uratibu wa Mradi(JCC) wa kuwajengea uwezo wakulima wadogowadogo wa umwagiliaji Awamu ya Pili ,TANCAID II wakifuatilia kwa makini mada zilizowasilishwa katika mkutano huo jijini Dodoma leo.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Wakulima katika zaidi ya skimu 100 za umwagiliaji nchini wamenufaika namafunzo ya kukuza na kuboresha kilimo cha umwagiliaji hivyo kuongezauzalishaji zaidi.
Akizungumza wakati wa mkutano wa Tano wa Kamati ya Pamoja yaUratibu wa Mradi wa kujenga uwezo kwa wakulima wadogowadogoAwamu ya Pili (TANCAID II) Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa
ya Umwagiliaji Bw. Marco Ndonde amesema wakulima walionufaika namafunzo hayo wanatoka kwenye Kanda zote nane za Umwagiliaji nchni nakuongeza kuwa mafunzo hayo yameleta matokeo makubwa katika sekta yaUmwagiliaji .
“Baada ya mafunzo hayo Wakulima katika skimu mbalimbali nchini sasa wana uwezo wa kuibua miradi inayowaletea faida na kuitekeleza kwaufanisi na hivyo kuongeza uzalishaji wa mazao yao” Alisema Bw. Ndonde.
Ndonde alisema mradi wa TANCAID II uliofadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Japan (JICA) tangu mwaka 2015 umejikita katika kujenga uwezo wa wakulima wadogo wadogo ambao ulitekelezwa na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) ukiwa na lengo la kukuza na kuboresha sekta ya umwagiliaji nchini.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi wa mradi wa TANCAID II Bw.Anthony Nyarubamba amesema chini ya mradi huo NIRC imetumia wataalamu wake kuandaa miongozo kabambe ya umwagiliaji (CGL)
ambayo imeanza kutumika na wakulima katika maeneo mbalimbali hususan katika skimu za umwagiliaji.
Kwa kutumia miongozo kabambe ya umwagiliaji, Nyarubamba amesema wakulima sasa wanaweza kusimamia skimu zao za umwagiliaji katika ngazi mbalimbali kuanzia uibuaji wa miradi hadi usimamizi wamiundombinu inayojengwa na serikali badala ya kuiacha iharibike kama ilivyokuwa awali.
Amesema moja ya mafanikio makubwa ya Mradi wa TANCAID II nikuwajengea uwezo maafisa kilimo, Wahandisi wa umwagiliaji wa Wilaya,Kanda na wakulima kwa ujumla katika maeneo ya uibuaji , utekelezaji,
uendeshaji na matunzo ya miradi husika.
Miongozo kambambe ya umwagiliaji, Nyarubamba amesema imewajengea wakulima uwezo wa kutunza taarifa ya uibuaji,utekelezaji,uendeshaji na matunzo ya skimu zao za umwagiliaji nakupanga mapema namna ya kutunza skimu hizo kabla hazijajengwa.Kutokana na kupewa mafunzo ya kutumia miongozo ya umwagiliaji,amesema wakulima wamekuwa na umiliki zaidi wa skimu zao, tofauti nahapo awali ambapo zilionekana kuwa haziwahusu ni mali ya serikali.
Akizungumza awali, Mhandisi Amy Mchelle amesema kutokana na kupata mafunzo wakulima sasa wanaweza kulipa asilimia tano ya mapato wanayopata baada ya uzalishaji.
Mhandisi Mchelle ameongeza kuwa miongozo kabambe ya umwagiliaji inawasaidia wakulima kupitia kamati za mradi, kusimamia ujenzi wamiundombinu ya umwagiliaji na kuzingatia ubora unaotakiwa.
Utumiaji wa miongozo kabambe ya umwagiliaji umesaidia kupunguza migororo itokanayo na utumiaji mbaya wa maji na ardhi katika skimu mbalimbali za umwagiliaji, amesema Mhandisi Mchelle.
“Miongozo imesaidia uboreshaji na utunzaji wa miundombinu ya umwagiliaji na kuwasaidia wakulima kupanga vizuri na kutekeleza nakufuatilia nakutathimini miradi wanayoianzisha” Alisema.
Mchelle amesema utumiaji wa miongozo ya umwagiliaji imewaongezea maarifa na ujuzi wa usimamizi wa rasilimali ikiwemo maji na kuongeza uzalishaji wa mazao mbalimbli wanayolima.
Naye Mshauri wa JICA nchini Bi. Namiko Yamada amesema kwa zaidi yamiaka 40 serikali ya Japan imetoa misaada kusaidia maendelea ya kilimohususan kilimo cha umwagiliaji.
Bi.Yamada amesema JICA chini ya mradi wa TANCAID II imewezakusaidia ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya umwagiliaji na kutoa mafunzo kwa vyama vya wamwagiliaji na wahandisi wa umwagiliaji.
Amesema JICA kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo pia imesaidia uendelezaji wa kilimo cha mpunga chini ya mradi wa TANRUCE2.

No comments:
Post a Comment