Na Veronica Kazimoto
Mkuu
wa Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga Kissa Kasongwa amewahimiza wananchi
kulipa kodi kwa wakati ili kuiwezesha Serikali kutekeleza miradi
mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma za jamii kwa lengo la
kuleta maendeleo nchini.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa Wiki ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi
inayofanyika wilayani humo, Mkuu huyo wa Wilaya amesema kuna miradi ya
huduma za jamii inayojengwa katika Wilaya ya Korogwe ikiwemo Hospitali
ya Wilaya, miradi ya barabara, maji, umeme na elimu ambayo yote
inategemea kodi ili iweze kukamilika.
“Bado
Korogwe kiwango chetu cha kulipa kodi ni kidogo kwani kati ya wananchi
303,000 wa wilaya hii, ni wananchi 2,800 ndiyo wanalipa kodi na
tumeshaelekeza kwamba wale wasiokuwemo kwenye mfumo wa TRA ambao mauzo
ghafi yao ni chini ya sh. 4,000,000 wanatakiwa kuwa na vitambulisho vya
wajasiriamali.
“Sote
tunatakiwa tutambue kwamba, tusipolipa kodi, tunajidhoofisha wenyewe
kimaendeleo. Hivyo, tujitahidi kulipa kodi kwa hiari na kwa wakati ili
tuweze kutekeleza miradi inayoendelea hapa wilayani kwetu,” alisema
Kasongwa.
Naye
Mkurugenzi wa Sheria wa Sekretariati ya Bodi na Huduma za Kisheria wa
TRA Makao Makuu Salim Beleko, amesema kuwa kodi ni sawa na damu kwenye
mwili wa binadamu, hivyo kama Serikali itashindwa kupata kodi itashindwa
kufanya jambo lolote la maendeleo kwa wananchi wake.
Aidha,
Beleko ameongeza kuwa wananchi hawatakiwi kulalamika kwasababu wanayo
fursa ya kukata rufaa endapo hawataridhika na makadirio ya kodi
waliyokadiriwa na malalamiko yao tatafanyiwa kazi Mamlaka ya Mapato
Tanzania huku akisisitiza kuwa Tanzania ni moja ya nchi chache ambazo
wananchi wake wanalipa kodi kwa hiari tofauti na nyingine ambapo
wanalipa kwa nguvu.
Kwa
upande wa Kaimu Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Lucas Kaigarula amesema
lengo la wiki hiyo ya huduma na elimu kwa mlipakodi ni kutoa elimu ya
kodi, kusikiliza malalamiko, changamoto pamoja na kupokea maoni
mbalimbali kutoka kwa walipakodi.
Wiki
ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi inafanyika nchi nzima ambapo kwa Mkoa
wa Tanga inafanyika wilayani Korogwe. Wiki hii ya elimu kwa mlipakodi
imeanza tarehe 13 na itamalizika tarehe 17 Mei, 2019 ikiongozwa na
kaulimbiu isemayo “Karibu tukuhudumie na tukuelimishe”.
Mkuu
wa Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga Kissa Kasongwa akizungumza kwenye
ufunguzi wa Wiki ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi katika Mkoa wa Tanga
inayofanyika katika Stendi ya zamani ya mabasi, Manundu. Wengine ni
Mkurugenzi wa Sheria wa Sekretariati ya Bodi na Huduma za Kisheria wa
TRA Makao Makuu Salim Beleko (kulia) na Kushoto ni Katibu Tawala wa
Wilaya ya Korogwe Rehema Bwasi
Mkurugenzi
wa Sheria wa Sekretariati ya Bodi na Huduma za Kisheria wa TRA Makao
Makuu Salim Beleko akizungumza kwenye ufunguzi wa Wiki ya Huduma na
Elimu kwa Mlipakodi inayofanyika katika Stendi ya zamani ya mabasi,
Manundu mkoani Tanga. Wengine ni Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Kissa
Kasongwa (kushoto) na Kulia ni Kaimu Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Lucas
Kaigarula.
Mkuu
wa Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga Kissa Kasongwa (wa kwanza kushoto)
akimsikiliza Ofisa wa Elimu kwa Mlipakodi Mkoa wa Tanga Salim Bakari
(kulia) kwenye ufunguzi wa Wiki ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi
inayofanyika katika Stendi ya zamani ya mabasi, Manundu mkoani Tanga.
(Picha na mpigapicha wetu).



No comments:
Post a Comment