Na. Vero Ignatus, Arumeru
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mhe John pombe magufuli anatazamia kuweka jiwe la msingi katika mradi wa uboreshaji wa huduma ya maji safi na usafi wa mazingira jijini Arusha na baadhi ya maneo ya wilaya ya Arumeru
Mradi huo uliotiliwa saini hivi karibuni utazinduliwa katika kijiji cha kimyaki majira ya saa nne asubuhi na baadae kuzungumza na wananchi katika kijiji cha mringarimga
Wakizungumzia hali ya maji, mkazi wa eneo mringaringa Josephat Joshua amesema wakinamama wanalazimika kwenda kutafuata maji ya kunywa kutoka mringaringa kilometa mbili katika sehemu inayoitwa njoro au kwa wavii.Wakati mwingine sisi wakina baba tunabakia na watoto nyumbani.
'' Wakinamama wanafuata maji, hadi arudi nyumbani anakuwa tayari amechoka sana kutokana na kutafuta maji umbali wote huo bado majukumu mengine yanamsubiria"alisema Joshua.
Bi Miriam Zakayo amesema inawalazimu kutembea umbali mrefu na kushindwa kutimiza majukumu yao kwa wakati
'' Maji tunayoayatumia ni ya mto nayo yanachukua muda mrefu hadi kufunguliwa kwa sababu wengine tunayatumia katika mifugo, mashamba, hivyo tukitaka maji ya kunywa tunayafuata mbali"alisema Miriam.
Mkazi mwingine wa kijiji hicho Saning'o Lebang'ute Laizer amesema kwa ujio wa Rais Magufuli kwao ni neema kwani itawatatulia tatizo hilo sugu la maji safi, barabara na umeme
''Tunashukuru sana kwa kuja kutufikia kwetu ni neema, barabara, hii inawahudumia watu wa kimmyaki, Ilikiding' a na Sambasha, mradi wa umeme, ni fursa kwetu pia"alisema Laizer.
No comments:
Post a Comment