Sunday, 2 December 2018

MTOLEA AELEZA SABABU ZA KUJIUNGA CCM,AWAONYA WANAOBEZA JUHUDI ZA SERIKALI KATIKA KULETA MAENDELEO



ALIYEKUWA Mbunge wa Jimbo la Temeke jijini Dar es Salaam Abdallah Mtolea amewaambia wajumbe wa Baraza la Hamashauri ya Manispaa ya Temeke kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) kuwa amefanya uamuzi sahihi kujiunga na Chama hicho.

Mtolea ambaye alikuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia Chama cha Wananchi(CUF)alitangaza kujiuzulu ubunge na nafasi zote ndani ya CUF siku za hivi karibuni akiwa Bungeni Mjini Dodoma.

Hivyo kwa sasa amejiunga na CCM na leo wakati anazungunza kwenye baraza hilo la halmashauri ya manispaa ya Temeke ameeleza kwa kina sababu za kuondoka CUF.Akifafanua zaidi wakati akifungua kikao cha baraza hilo Mtolea amesema uamuzi sahihi kurudi CCM katika kuendeleza na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora katika kila sekta nchini.

Amebainisha kuwa wapinzani wapo kwa ajili ya kupinga juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano na kazi kubwa ni kubeza na kushawishi vijana kufanya ushabiki ambao hauna manufaa kwa maslahi ya nchi na Taifa kwa ujumla.Pia Mtolea amezungumzia wasanii ambapo amesema hawajakatazwa kufanya kampeni bali wasanii wa Mkoa husika wapatiwe vipaumbele katika kuonesha vipaji vyao.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana Kata ya Temeke kupitia CCM Fadhili Faungo amesema kuwa Rais Dk.John Magufuli amekuwa anashirikiana bega kwa bega na vijana kwani anaamini vijana ndio nguvu kazi ya Taifa .Pia amesema lengo la kukutana kwa wajumbe wa Baraza hilo ni kuangalia miradi ya maendeleo ambayo itatekelezwa kupitia fedha ambazo zimetolewa na Serikali.

Wakati huo huo imeelezwa kuwa baadhi ya wajumbe wameshawasilisha mawazo yao katika matumizi ya kufungua biashara ambazo zitaleta chachu ya kuongeza pato la Taifa.
ALIYEKUWA Mbunge wa Jimbo la Temeke jijini Dar es Salaam Abdallah Mtolea akizungumza mbele ya Wajumbe wa Baraza la Hamashauri ya Manispaa ya Temeke kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) kuwa amefanya uamuzi sahihi kujiunga na Chama hicho.

No comments:

Post a Comment