Rais
wa Tanzania, John Magufuli na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta
wanatarajiwa kufungua Kituo cha Forodha cha Pamoja (OSBP) eneo la
Namanga upande Kenya na Tanzania kisha kufuatiwa na sherehe ya uzinduzi
huo zitakazofanyika upande wa Tanzania.
Viongozi
mbalimbali wakiwemo mawaziri, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama,
wabunge na viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wapo upande wa
Kenya kwa ajili ya uzinduzi huo unaofanyika leo Jumamosi Desemba 1,
2018.
Lengo la kuanzisha OSBP ni kurahisisha huduma na watu kuchukua muda mfupi kupata huduma za Forodha mpakani.
Kituo
cha Forodha cha Namanga ni moja ya vituo vinavyotumika kutoka na
kuingia Kenya mkoa wa Arusha, kituo kingine kidogo ni Osmolo kilichopo
wilayani Ngorongoro.
No comments:
Post a Comment