
WAKATI baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika wilaya na mikoa mbalimbali, wakipita kuwahamasisha wanachama wenye nafasi za uongozi ndani ya chama kuwania nafasi za ubunge na udiwani hatimaye uongozi wa juu wa chama hicho umetoa tamkoa na kuzuia mpango huo.
Hilo limekuja wakati huku baadhi ya viongozi wa wilaya wakihamasisha wanachama kujitokeza kuwania nafasi za uongozi ikiwamo ubunge na udiwani hasa kwa wenyeviti wa wilaya na kata pamoja na jumuiya zake na pindi wataposhinda wataachia nafasi walizonazo ndani ya chama.
Kutokana na hali hiyo CCM kimeonya wanachama wake wenye nia ya kuwania ubunge na udiwani kwa kuwataka kufuata utaratibu uliowekwa na chama hicho.
No comments:
Post a Comment