Mbunge
wa Kilombero (Chadema), Peter Lijualikali, ameibuka na kutaja sababu
inayoweza kumshawishi kujiunga na chama tawala hicho.
Akizungumza
na waandishi wa habari, muda mfupi baada ya kukagua mradi wa reli ya
kisasa (SGR), kipande cha Dar es Salaam-Kilosa, akiwa miongoni wa
wabunge wa kundi la maendeleo endelevu bungeni walioutembelea,
Lijualikali alisema anaweza kuihama Chadema na kujiunga na CCM ikiwa
serikali itaendelea kutekeleza miradi mikubwa kama huo.
“Wanaosema
nitahamia CCM ni jambo jema kuwa wanapenda nihamie CCM, ila nitahamia
CCM kama tu nitaona kuna sababu za msingi na mengine ya msingi
yanafanyika," alisema.
Lijualikali
alisema kuwa kama serikali itaendelea kutekeleza miradi mingine mikubwa
nchini, hatakuwa na sababu za kukataa kukihama chama chake.
Hata hivyo, mbunge huyo alisema anakwazwa na kitendo cha kutishwa na kukamatwa kamatwa kwa viongozi wa upinzani nchini.
"Nitahamia
CCM kama nitaona sababu za msingi sana na mengine ya msingi, lakini si
huku kutishana na kufungwa fungwa na kufia jela," alisema Lijualikali.
Alisema hayuko Chadema kwa bahati mbaya na anaamini kwa sasa ni sehemu sahihi kuwapo.
Akizungumzia
mradi huio, Lijualikali alisema: "Mradi huu ni kitu endelevu, kitu
ambacho tunaamini hata Chadema tukichukua nchi, hatutaing'oa reli,
itabaki."
Alisema mafanikio ya mradi huo yataonekana mara utakapokamilika nchi nzima na mizigo kuanza kusafirishwa kwenda nchi mbalimbali.
Alisema mafanikio ya mradi huo yataonekana mara utakapokamilika nchi nzima na mizigo kuanza kusafirishwa kwenda nchi mbalimbali.
“Baada
ya mizigo kuanza kusafirishwa, nchi itapiga hatua kubwa kiuchumi na
uchumi wa mwananchi mmoja mmoja utakua," alisema Lijualikali.
Alishauri
serikali kujenga barabara za kiwango cha lami kuunganisha na stesheni
za reli mpya ya kisasa.“Mradi huu utapendeza kama zitajengwa na barabara
za kiwango cha lami kwa ajili ya kuunganika na stesheni za reli, hivyo
kurahisisha maisha ya watu," alisema.
No comments:
Post a Comment